Maofisa Elimu kata ktk H/W ya Babati wametakiwa kufanya Kazi ya kusimamia taaluma na kuyatekeleza kwa bidii ili kuinua kiwango chá Elimu na kufikia kiwango chá ufaulu wa asilimia 90 kilichowekwa na Mkoa wa Manyara kwa mwaka 2018.Hayo amesema Afisa Elimu Mkoa wa Manyara Ndg. Arnold S.Msuya Katika kikao cha Maofisa Elimu Kata kilichofanyika leo ktk ukumbi wa H/W ya Babati kwa ajili ya kufanya tathimini ya Matokeo ya Mitihani ya darasa lá nne, drs Sabá, kidato cha Pili na kidato cha nne mwaka 2017 na kuweka mikakati Kwa mwaka 2018. Afisa Elimu huyo amesisitiza Maofisa Elimu kata kuwasimamia Walimu kwa karibu kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kuwalinda wanafunzi dhidi ya mateso. Kikao hicho pia kimehudhuliwa na Maofisa Elimu Msingi na Sekondari, Maofisa Elimu Udhibiti ubora na Maofisa Tume ya ya Watumishi wa Walimu (TSC) ambapo mada na maelekezo mbalimbali yametolewa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.