Katika jitihada za serikali za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma nzuri za afya kwa haraka na karibu na eneo anakoishi, Kituo cha Afya cha Bashneti katika kimenza kutoa huduma. Akizungumza kwa furaha leo mbele ya Wataalam wa Afya , Diwani wa Kata ya Bashnet Mhe. Jovita Mandoo amesema " Ninayo furaha kuona kituo hiki kikubwa cha aina yake kimenza kutoa huduma ,Pongezi nyingi kwa Serikali hasa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa Afya hasa kata Bashnet .Naye Daktari Kiongozi Dk Hosea Madama amesema kituo hicho kimeanza kazi na kitakuwa mkombozi mkubwa kwa kata zilizoko ukanda wa juu wa Bashnet wananchi wote wanakaribishwa. Kituo cha Afya Bashnet kinajengwa na fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kushirikiana na Wananchi, serikali kuu na wadau wa Afya.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.