Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Babati ameanzisha utaratibu wa kukagua shule za Msingi na Sekondari kuangalia utaratibu wa ufundishaji wanafunzi Shuleni. Akiongea na Walimu wa shule za Msingi Bacho na Shule ya Sekondari Utwali zilizoko Tarafa ya Bashnet kwa nyakati tofauti amesema Walimu Wanatakiwa kujituma kwa nguvu zote kuhakikisha watoto wanapata Elimu bora kwa kufuata miongozo iliyotolewa na serikali.Walimu kwa upande wao wameshukuru utaratibu huo na kuomba uendelee kwani unasaidia kutatua changamoto katika sekta ya Elimu na kuinua kiwango cha ufahulu.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.