Diwani wa kata ya Madunga Mhe. John S. Noya amechaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa Kipindi cha tatu mfululizo. Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. Nicodemus Tarmo amesema Mhe. John Noya ( CCM) ameshinda Kwa kupata Kura 19 dhidi ya mpinzani wake Prosper Temu( CHADEMA) aliyepata kura 14.Wajumbe wamepongeza Uchaguzi huo kuwa umefanyika Kwa amani na kufuata taratibu zote za Baraza hilo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.