Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg Halfan Matipula amewashukuru Wafadhili kwa ujenzi wa Shule ya sekondari ya The Tara Getty. Katibu Tawala ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa ujenzi wa Awamu ya tatu wa Shule ya Sekondari ya The Tara Getty iliyoko Kata ya Magara H/ Wilaya ya Babati inayojengwa na shirika lisilo la kiserikali la African Foundation. "kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Babati tunashukuru sana Kwa ujenzi wa Shule hii tangu mwanzo mpaka leo tunapoelekea ujenzi wa Awamu ya tatu tunasema asanteni sana na Ushirikiano huo uendelee" amesisitiza kiongozi huyo" Katika Awamu hii ya tatu Shirika la African foundation limetoa tsh 500 Million kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili na bwalo moja la chakula katika Shule ya Sekondari The Tara Getty.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.