Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Ndg.Maryam Muhaji ameipongeza H/W ya Babati kwa ukusanyaji wa Mapato na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.Hayo ameyasema leo kwenye Ukumbi wa H/Wilaya ya wakati alipotembelea H/W hiyo kukutana na timu ya menejimenti,kujitambulisha na kufuatilia utendaji kazi wa taasisi.Ndg Muhaji amesema "nawapongeza viongozi watumishi na madiwani kwa ukusanyaji wa mapato mpaka kufikia asilimia 57 kwa mwaka wa fedha2023/2024 naomba ushirikiano huo uendelee'amesisitiza kiongozi huyo Wakati huo huo ameiambia timu ya menejimenti kusimamia vipaumbele vyake vinne ili kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi. Ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni ukusanyaji wa Mapato ufike asilimia 100, ujenzi na usimamizi wa miradi iendane na thamani ya fedha tolewa, kutatua kero za wananchi na matumizi bora ya fedha za serikali.Aidha amesisitiza timu ya menejimenti kujenga mahusiano mazuri na watumishi,taasisi,viongozi na wananchi.Naye Mkurugenzi Mtendaji Anna Mbogo ameshukuru na kuhaidi maagizo yote yatatekelezwa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.