Halmashauri zimetakiwa kukusanya mapato yake ya ndani ili kukamilisha miradi ya maendeleo. Hayo yamesemwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali za Mitaa(LAAC) Mhe. Ester Bulaya leo wakati kamati hiyo ilipokagua miradi ya Jengo la Utawala na Nyumba ya Mkurugenzi H/ Wilaya ya Babati." Hakikisheni mnaongeza mapato ya ndani ili fedha hizo zisaidie kukamilisha miradi ya maendeleo kuliko kutegemea fedha zote zitoke serikali kuu" amesisitiza kiongozi huyo . Wakati huohuo wameagiza Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara kutimiza wajibu wao kwa kusimamia na kufuatilia ujenzi wa miradi ili iendane na thamani ya fedha inayotolewa na serikali. Naye Mkurugenzi wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo ameishukuru kamati hiyo kutembelea miradi na kueleza maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi kwa wakati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.