Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Manyara imetembelea, kukagua,kuridhishwa na kupongeza utekelezaji wa Ilani wa ujenzi wa miradi mitatu yenye thamani ya Tshs 1,504,747,466 katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake Bi Fatuma Hassan Tsea kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa ameyasema hayo leo Shule ya msingi Gallapo mara baada ya ukaguzi wa utekelezaji ilani ya CCM katika Halmashauri ya wilaya ya Babati "Tumekagua miradi yote mitatu ,tumeridhishwa na ujenzi wa miradi yote na tunawapongeza sana" amesisitiza kiongozi huyo. Miradi iliyokaguliwa na kamati ya siasa mkoa katika H/W Babati ni utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Afya Dareda Kati wenye thamani ya Tshs 935,058,394 ujenzi wa Skimu ya Maji Boay wenye thamani yaTshs 373,949,072 na Ujenzi wa Madarasa 5 mapya na ukarabati wa madarasa 7 na jengo la Utawala katika shule ya Msingi kongwe ya Gallapo. Naye Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Lazaro Twange ameshukuru kamati hiyo na kuahidi kutekeleza maagizo yote.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.