Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limesisitiza Wananchi kuendelea kuchangia chakula ili watoto wao wa shule za Msingi na Sekondari wapate chakula cha mchana shuleni.Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe Nicodemus Tarmo kwenye Mkutano wa siku ya Kwanza wa kujadili taarifa za kata uliofanyika katika Ukumbi wa H/Wilaya ya Babati ya (zamani.)
"Inashangaza jamii wanachangia chakula kwa ajili ya Wanafunzi wa sekondari lakini kwa Wanafunzi wa shule za Msingi wanakataa, hivyo Baraza linaelekeza jamii kuendelea kuchangia chakula kwa Wanafunzi wote kama mwongozo wa Elimu bila malipo wa mwaka 2016 unavyoelekeza"amesisitiza kiongozi huyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.