Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kupata Daraja A la Alama 81.1 katika tathimi ya jumla ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwaka 2021/2022. Mkuu wa Wilaya ya Babati amesaema hayo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati uliofanyika leo Makao makuu ya H/Wilaya" Kwa mujiba taarifa ya Waziri wa Nchi OR_TAMISEMI Halmashauri yetu imepata Daraja A katika tathmini ya jumla ya Utendaji, Hongereni sana" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amesisitiza Halmashauri ya Wilaya kuendelea kutenga na kupeleka fedha ya asilimia 10% kwenye mfuko wa Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuongeza wigo wa makusanyo ya mapato ya ndani.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.