Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepongezwa kwa ujenzi na usimamizi wa miradi ya Afya na usafi wa mazingira kwenye shule za msingi na vituo vya kutolea huduma. Hayo yamesemwa na Timu ya ukaguzi inayojumuisha wajumbe kutoka Bank ya Dunia, Wizara za Afya, TAMISEMI na Wizara ya maji waliofika leo kukagua miradi H/ Wilaya ya Babati katika shule ya Msingi Kwaraa Kata ya Endakiso na Zahanati ya Minjingu kata ya Nkait" Sisi kama Timu tunapongeza uongozi kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri uliopelekea ujenzi bora wa miradi ya WASH na SHWASH". Wamesisitiza wajumbe hao .Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo ameshukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha na kuweka mazingira wezeshi ya wafadhili kuweza kutoa fedha kujenga miundombinu mbalimbali katika shule za msingi na vituo vya kutolea huduma kwa wananchi wa H/ Wilaya ya Babati. Katika kata ya Endakiso ambapo choo cha matundu19 chenye thamani ya tshs 52, 349,006 katika shule msingi Kwaraa kimejengwa, Diwani wa Kata hiyo Mhe.Hasan Dodo ametoa shukurani kwa serikali na wafadhili kwa ujenzi wa mradi huo katika kata yake. Miradi wa SWASH na WASH inahusika na ujenzi wa matundu ya vyoo, Matanki ya maji, Vichomea taka vinawia mikono na uvunaji wa maji ya mvua katika shule za Msingi na vituo vya kutolea huduma katika H/ wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.