Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amepongeza Baraza la Madiwani,Timu ya Menejimenti naWatumishi wa H/W ya Babati kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu Mfululizo, 2020/2021,2021/2022 na mwaka 2022/2023. Akiwasoma hotuba hiyo leo iliyowasilishwa na Katibu Tawala Mkoa waManyara Bi Maryam Muhaji kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG) kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, 2023 uliofanyika katika ukumbi wa H/Wilaya. KatibuTawala Bi.Muhaji amesisitiza pamoja nakupata hati safi,menejimenti ihakikishe maeneo yaliyotajwa kuwa na mapungufu katika taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za serikali kwa mwaka 2022/2023 yanafanyiwa kazi kikamilifu ikiwemo kujibu hoja za nyuma pamoja na maagizo ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa( LAAC)Kwa upande wake M/kiti wa H/Wilaya ya Babati Mhe.John Noya ameshukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi serikali kwa ushauri na kuahidi kutekeleza maagizo yote.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.