Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepata hati inayoridhisha katika Ukaguzi wa hesabu za mwaka 2016/2017.Akitoa taarifa za serikali kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri,Katibu wa kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg. Hamisi Idd Malinga amesema Halmashauri imepata hati inayoridhisha na maelekezo machache ya kuzingatia. Naye Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. Nicodemus Tarmo amesema wamepokea taarifa hiyo kwa furaha na kuwataka Watendaji wa Halmashauri hiyo wasibweteke na hati hiyo bali waendelee kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili mwaka wa fedha 2017/2018 iweze kufanya vizuri zaidi
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.