Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara inatarajia kukusanya na kupokea jumla ya Kiasi cha Tsh 41,821,134,310 kwa Mwaka wa fedha 2019/2020. Akiwasilisha Makisio ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwenye Mkutano Maalum wa Baraza Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ndg Benitho Kavenuke amesema Bajeti hiyo ikipitishwa inategemea kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Halmashauri ya Babati.Diwani wa Kata ya Mamire ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe Nicodemus Tarmo ameomba Madiwani washirikiane na Wakuu wa Idara kutambua vyanzo vipya vya Mapato katika maeneo yao ili kuongeza Mapato ya Halmashauri kuliko kuendelea kutegemea chanzo kimoja cha ushuru wa Mazao. Baraza hilo limejadili na kupitisha kiasi cha Tsh 41,821,134,310 ikiwa ni fedha kutoka Mapato ya vyanzo vya ndani,Matumizi ya Kawaida,Mishahara na Miradi ya Maendeleo kikusanywe na kitumike kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.