Halmashauri ya Wilaya ya Babati imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika mashindano ya UMITASHUMTA ya Mwaka 2023.Akitangaza matokeo ya Mashindano hayo jana katika viwanja vya shule ya Msingi Katesh A, Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Elimu Mkoa Ndg Halfan Masukira amesema Halmashauri ya Wilaya ya Babati imekuwa ya kwanza katika mashindano hayo na kuchukua vikombe sita katika fani za Riadha wanawake, Riadha wanaume,Riadha Jumla,Netiboli, Mpira wa Miguu wanawake na Ushindi wa Jumla . Wakati huo huo Masukira amewapongeza vijana wote kutoka Halmashauri 7 za mkoa wa Manyara kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo . Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Benedict Ntabagi akipokea vikombe hivyo leo kutoka kwa Afisa Elimu msingi Ndg Kavishe amewapongeza vijana kufanya vizuri kwa katika mashindano hayo na akasisitiza kuongeza bidii na kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya Kitaifa. Vijana 21 kutoka Halmashauri ya Wilaya wameteuliwa kuunda timu ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA taifa Juni Mkoani Tabora.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.