Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi ya Wilaya ya Babati imepongeza H/Wilaya ya Babati kwa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa ujenzi mzuri na wenye tija wa miradi ya Maendeleo.Hayo wamayasema leo kwa nyakati tofauti katika ukaguzi wa miradi katika Kata za Nkait,Kisangaji,Nar, Madunga Magugu na Qameyu katika siku yao ya kwanza ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM."Tumekagua na kujiridhisha miradi imejengwa kwa kiwango tunawapongeza sana" Amesisitiza mjumbe Ndg John Geu .Aidha wamepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya serikali na chama cha Mapinduzi. Katika ukaguzi huo wamejionea miradi ya sekta mbalimbali na kushiriki na wananchi katika ujenzi .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.