Wasimamizi wa fedha katika ngazi za Vijiji,Zahanati,Vituo vya Afya na Shule wametakiwa kufuata taratibu za Manunuzi, sheria na kanuni katika Matumizi ya fedha za Serikali.Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Dkt Hosea Madama kwenye Mafunzo ya Manunuzi, Mapato na Matumizi ya fedha Serikali kwa Watendaji wa Vijiji ,Wahasibu wa vituo vya Afya ,zahanati shule za Msingi na Sekondari yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri yaWilaya ya Babati " Baada ya mafunzo haya kila mmoja afuate taratibu na sheria za Manunuzi na fedha kwani ukaguzi utafanyika kila baada ya miezi mitatu" amesisitiza Kaimu Mkurugenzi. Aidha ameagiza Mkaguzi wa ndani kila mwezi kukagua baadhi ya shule , vituo vya afya na zahanati ili watakaogundulika kwenda kinyume na taaribu za fedha hatua zichukuliwe kwani wamepewa mafunzo ya kutosha. Naye Mtendaji wa Kijiji cha Gichameda Ndg John Haymora kwa niaba ya Washiriki ameshukuru Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kutoa mafunzo hayo na kueleza kuwa wataenda kutekeleza na kufanya kama walivyoelekezwa na Mweka Hazina , Afisa ugavi na Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri Wilaya na matokea yatakuwa makubwa. Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Washiriki 330 kutoka Kata zote 25 za Halmashauri ya Wilaya ya Babati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.