Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kujiendeleza Kielimu ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa na kuwaeletea wananchi Maendeleo .Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Iddi Malinga kwenye Kikao maalum cha Baraza la Wafanyakazi la kupitia mapendekezo ya Makisio ya Mapato na Matumizi ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa Mwaka 2020/2021 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya. "Elimu inalipa nendeni mkasome mjiongezee Maarifa ili msaidie wananchi kutatua changamoto zao" amesisitiza Mkurugenzi huyo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.