Shule ya Sekondari Sarame inayojengwa Serikali Ktk Kijiji Cha Magagu Kata ya Magugu Kwa mara ya kwanza imeanza kupokea wanafunzi wa Kidato Cha kwanza leo trh 9/01/2023. Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Ndg Anna Mbogo ameshiriki ufunguzi Shule hiyo na kuwataka wanafunzi hao kutunza miundombinu ya Shule na akawaomba Wananchi wa Kata ya Magugu kushiriki shughuli za Maendeleo ya Shule hiyo. Shule hiyo inajengwa na Serikali kuu kupitia Mradi wa SQUIP Kwa kushirikiana na Wananchi wa Kata ya Magugu na H/ Wilaya ya Babati na ujenzi wa Shule hiyo unaendelea .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.