Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Lazaro Twange amepongeza shule za sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha Nne 2023. Mhe Twange ameyasema hayo leo kwenye hafla ya kukabidhi vyeti vya pongezi iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Ayalagaya " Napongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Babati, wakuu wa shule na walimu wote waliowezesha wanafunzi kufanya vizuri mwaka huu" amesisitiza kiongozi huyo" Mhe Twange ameongeza na kusema Nimekoshwa kwa shule nyingi kufuta zero , ambapo ni wanafunzi 16 tu waliopata daraja 0 kwa shule zote za H/ Wilaya ya Babati. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewapongeza walimu Wote na kuwataka walimu hao kuweka mikakati madhubuti ya kutokomeza daraja 0 kwa mtihani wa mwaka 2024
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.