Mkuu wa Babati.Mhe Elizabeth Kitundu kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga wamewashukuru wafadhili wa Mashirika ya Habitat for Humanity,Water Aid na Wananchi wa kijiji cha Sangara kata ya Riroda H/W ya Babati kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji. Wakiongea kwa nyakati tofauti kwenye hafla fupi ya kuweka jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji wa Sangara ulioko ktk Kijiji cha Sangara wamesema wanawashukuru Wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na wananchi kuweza kujenga mradi wa Maji mkubwa ambao utawezesha wananchi wa kijiji cha Sangara kupata Maji safi na kujiletea maendeleo."Tunawashukuru sana Wadau wetu wa maendeleo kwa kuleta mradi mkubwa wa Maji hapa Sangara ,naomba wananchi kulinda na kuitunza miundombinu yote ya Maji ya mradi huu",amesisitiza Mkuu wa Wilaya ya Babati.Naye Mkurugenzi wa Shirika la Habitat for Humanity Ndg Sairas Watuku ameshukuru Serikali na wananchi kwa ushirikiano wao .Mradi huo utagharimu kiasi Tsh 210 Million.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.