Bank ya NMB tawi la Babati imetoa msaada wa vifaa vya Zahanati na shule vyenye thamani ya Tsh 15,000,000 kusaidia jitihada za jamii katika sekta ya Elimu na Afya kwa Zahanati ya Kijiji cha Gesbert na Shule ya Msingi Getara kata ya Duru na Shule ya Msingi Ayatlaa Kata ya Riroda katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati .Akikabidhi vifaa hivyo leo kwenye Zahanati ya Kijiji cha Gesbert na Shule ya Msingi Ayatlaa kwa nyakati tofauti kwa Mgeni Rasmi Mhe. Elizabeth Kitundu Mkuu wa Babati , Meneja wa NMB Kanda ya Kati Ndg Nsolo Mlonzi, amesema Msaada huo unatokana na faida walioipata kutoka kwa wateja wake hivyo wanarudisha ili isaidie jitihada za jamii kujiletea maendeleo katika sekta za Elimu na Afya. Naye Mgeni Rasmi kabla ya kukabidhi Vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Babati amewashukuru na kuwapongeza NMB kwa msaada walioutoa na kutoa Wito kwa NMB kuendelea kutoa msaada katika sekta za Elimu na Afya na kusisitiza Wananchi wengi kwenda Bank ya NMB kufungua akaunti ili ipate wateja wengi zaidi na kusaidia jamii.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Malinga akipokea Vitanda 5 vya kawaida,Mashuka 54 na Kitanda kimoja cha Kujifungulia Wajawazito vya Zahanati ya Gesbert katika Kijiji cha Gesbert na kupokea Bati 106, Mbao 136, Misumari Kg 18 na Gypsam 18 vya Shule za Msingi ( Ayatlaa na Getara) vyote vikiwa na thamani ya Tsh 15 Millioni kutoka kwa Mgeni Rasmi amewashukuru Bank ya NMB na kusema vifaa hivyo vimefika wakati muafaka na kuahidi vifaa hivyo kuvitunza ,kuvisimamia na kuhakikisha vinafanya kazi
iliyokusudiwa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.