Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limepongeza Walimu wa Shule za Sekondari zilizofanya vizuri kwa matokeo ya mtihani wa kidato Cha nne Kwa mwaka 2022 yaliotangazwa hivi karibu na Baraza la Mtihani. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amesema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati. " Shule nyingi zimefanya vizuri mwaka huu zikiongozwa na Shule ya Sekondari Ayalagaya, Dareda, Madunga, Masabeda na nyingine ambapo kwa ujumla wanafunzi 3172 wamefaulu kati ya watainiwa 3218 waliofanya mtihani sawa na asilimia 98.6. Walimu na Bodi za Shule wapokee pongezi nyingi". amesisitiza kiongozi huyo. Aidha Baraza la Madiwani limempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg Anna Mbogo kwa usimamizi na kufanya mabadiliko makubwa ktk Shule za sekondari ambako kumepelekea kupanda kwa taaluma katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.