Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Mhe. John Noya amewaagiza Watumishi kuhakikisha wanakusanya mapato ya ndani kwa vyanzo vilivyokisiwa ili kupata fedha za ujenzi wa miradi ya Maendeleo. Hayo ameyasema leo kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani la kujadili Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2021/2022 uliofanyika leo katika makao Makuu ya Halmashauri Kijiji cha Loto Kata ya Dareda."Watumishi jipangeni vyema kuhakikisha kila chanzo kilichokisiwa kinakusanywa na fedha hizo zinatumika ktk miradi ya Maendeleo" Amesisitiza. Awali Mkurugenzi Mtendaji wa H/W ya Wilaya ya Babati Ndg John John Nchimbi amewasilisha Makisio ya Mpango na Bajeti wa H/W kwa mwaka 2021/2022 na kusema katika mwaka huo H/W inategemea kukusanya fedha na kupokea Tsh 54,457,810,186,000 na kutumia kiasi hicho ktk ujenzi wa Miradi na shughuli mbalimbali ambapo Tsh 2,934,996,000 ni mapato kutoka vyanzo vya ndani . Katika kikao hicho wajumbe wamesisitiza wadau wa Maendeleo na Wananchi washirikishwe vyema.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.