Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati limeagiza maeneo yote ya taasisi yaliyoko Vijijini yapimwe na kupata hati ili yalindwe kisheria na kuzuia wavamizi. Mwenyekiti wa H/ Wilaya ya Babati Mhe. John Noya ameyasema hayo leo kwenye Mkutano wa Baraza la kwanza la Madiwani la kujadili taarifa za Kata lililofanyika leo ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati - Arri " Kwa mwaka huu tumedhamilia maeneo yote ya taasisi zetu yapimwe ili kuzuia wavamizi na kuzuia migogoro mbalimbali ya ardhi" amesisitiza kiongozi huyo. Mhe. Noya ametaja maeneo ya taasisi hizo kuwa ni Shule za Msingi na Sekondari, Ofisi za Kata na Vijiji, maeneo yote ya zahanati, Hospitali na vituo vya Afya yote yapimwe.Wakati huo huo Baraza la Madiwani limeagiza Bodi ya Shule ya Sekondari ya Dareda na Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Dareda kukaa pamoja kutambua na kutatua migogoro ya mipaka ya Shule hiyo. Mhe Noya ameagiza taasisi zote kutafuta fedha kiasi chaTsh 300,000 kwa ajili ya kugharamia upimaji huo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.