Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Babati lapongezwa kwa kupata hati Safi ya Ukaguzi wa mahesabu ya fedha ya mwaka 2016/2017.Akisoma Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwenye kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kujadili taarifa ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwaka 2016/2017 Mwakilishi wake Ndg Arnold M.Msuya amesema"anapongezaza Baraza na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya Babati kwa kupata hati Safi na kulitaka Baraza kuendelea kusimamia Menejimenti kikamilifu kutimiza wajibu wake" Amesisitiza.Aidha amewataka wakuu wa Idara kudhibiti hoja na kila mkuu wa Idara, kitengo na sehemu ni lazima awajibike na kushiriki kikamilifu wakati wa Ukaguzi, badala ya utaratibu wa sasa wa kuiachia Idara ya fedha jukumu la kutafuta majibu wakati wa Ukaguzi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.