Shule ya Msingi Dareda Kati iliyoko H/ Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imeshika nafasi ya tatu kitaifa kwa kuwa na Vyoo bora na kisasa ktk Mashindano ya Taifa ya Afya na Usafi wa Mazingira kundi la Shule za Msingi Tanzania Bara.Afisa Afya wa H/ Wilaya Ndg Susten Mwabulambo na Mwl Mkuu wa shule hiyo Ndg Samwel Sangwa wamepokea Cheti cha ushindi kwa Shule hiyo kutoka kwa Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.Dkt Dorothy Gwajima leo katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maofisa Afya , Mazingira na usafi mjini Dodoma.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.