Friday 27th, December 2024
@uwanja wa kwaraa
Mkuu wa Mkoa waManyara Mhe. Dkt Joel Bendera amesisistiza uajibikaji na uadilifu mahali pakazi. Mkuu wa Mkoa huyo ameyaeleza hayo katika siku ya Wafanyakazi Meimosi Iliyofanyika Mjini Babati katika uwanja wa Kwaraa,"Fanyeni kazi kwa bidii, jiepusheni na Uvivu, majungu na uzembe mahali pa kazi" alisistiza Mkuu wa Mkoa. Akijibu Risala ya Wafanyakazi iliyoandaliwa na Muungano wa Vyama vyawafanyakazi TUCTA Mkoa wa Manyara, Mkuu wa Mkoa amesema waajiri wanaokataza Kuunda vyama vya wafanyakazi waache mara moja, Aidha ameahidi kukaa na waajiri na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ili kutatua kero zote za wanyakazi wa Mkoa wa Manyara. Mkuu wa Mkoa amesitiza watumishi wote kulinda amani kwani ndio kigezo kikubwa cha kuleta maendeleo. Sherehe hizo zilihudhuriwa na umati mkubwa wa watumishi, wanachi na viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa, Wilaya na wafanyakazi hodari walitunukiwa zawadi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.