Friday 9th, May 2025
@Kata ya Madunga
Timu ya ya Ukaguzi na ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI na Wizara ya Fedha na Mipango, imewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ujenzi wa miradi ya Maendeleo kwa nguvu zao wenyewe. Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Timu hiyo Ndg Idrisa Mtandi ambaye ni Mchumi Ofisi ya Raisi TAMISEMI wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika kata za Magugu,Ufana, Bashnet,Madunga,Dabil,Duru na Dareda katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati
Amesema timu imeridhishwa na miradi iliyokaguliwa iliyojengwa kwa michango ya wananchi na serikali na kaendelea kuwaomba kuendelea kutoa michango yao kukamilisha miradi inayoendelea kujengwa. Naye Diwani wa Kata ya Madunga Ndg. Noya John Silvin kwa niaba ya Wananchi aliishukuru Serikali kwa kutoa fedha kusaidia nguvu za Wananchi kukamilisha miradi ya maendeleo. Miradi iliyokaguliwa na Timu hiyo ni miradi iliyoka kwenye sekta ya Elimu,Afya na Maji.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.