Friday 27th, December 2024
@
Kata na Vijiji waliofanya vizuri katika kuhamasisha Kaya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa iCHF wamepewa Zawadi katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya lililofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya tarehe 05/5/2017 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya-Babati Mhe. Nicodemus Tarmo alisema kwa utaratibu wa Bima ya Afya Mkoa iliyojiwekea kuwa kila kipindi cha Miezi 3 (Robo mwaka) lazima apatikane mshindi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa (iCHF.) Walioshinda nafasi ya Kwanza ni; Kata ya Magara alipata (7.1%) na kuzawadiwa Tsh 100,000 na ngao pamoja na Kijiji cha Magara kilichopata zawadi ya Tsh 50,000. Mshindi wa pili ni Kata ya Madunga (7%) na Mshindi wa tatu ni kata ya Kisangaji.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.