Friday 27th, December 2024
@Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Dkt. Joel N. Bendera amewaagiza wakuu wa Idara na Vitengo wa H/Wilaya ya Babati kuwa kila Mkuu wa Idara na Vitengo awajibike na kusiriki kikamilifu wakati wa ukaguzi badala ya utaratibu wa sasa wa kuiachia Idara ya Fedha jukumu la kutafuta majibu wakati wa Ukaguzi na Halmashauri kuonesha uhodari wa kujibu hoja zinazojitokeza badala ya kuzuia hoja.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kwenye kikao Maalum cha Baraza la madiwani cha kujadili ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali (CAG) mwaka wa fedha 2015/2016 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa H/Wilaya. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa kila Mkuu wa Idara na Vitengo awajibike kwa nafasi yake kwani hutumia fedha kama zinavyoidhinishwa na Baraza la Madiwani. Awali akifungua kikao Mwenyekiiti wa Baraza la Madiwani Mhe, Nicodemus Tarmo aliwaeleza wajumbe kuwa katika ukaguzi wa wa mahesabu ya fedha mwaka 2015/2016 Halmashauri ya Wilaya ya Babati imepata hati safi. Pamaoja na Halmashauri ya Wilaya Kupata Hati safi, Mkuu wa Mkoa alisistiza Mambo makuu matatu kufanyiwa utekelezaji wa haraka ambayo ni Kukosekana kwa uthibitisho wa marejesho ya Mishahara isiyolipwa kutoka Bank kwenda Hazina Tsh 13,769,238,689,Malipo yaliyofanyika kwa Wadai pasipo madeni hayo kuoneshwa kwenye vitabu vya hesabu vya Halmashauri Tsh 3,295,858 na Malipo ya Mishahara kwa watumishi ambao sio wa Serikali Tsh 11,292,277.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.