Friday 9th, May 2025
@
Kituo cha afya ufana
Jengo la maabara katika shule ya sekondari masabeda
Timu ya Tathimini na ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya Babati imetembelea Miradi ya maendeleo inayojengwa kwa nguvu za wananchi, Halmashauri Wadau wa maendeleo na Serikali kuu kupitia fedha cha Maendeleo za (CDG)
Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa Wodi ya Wakina Mama katika kituo cha Afya Ufana, Ujenzi wa Vyumba vya Maabara katika shule za sekondari, Ndeki kata ya ufana, Endamanang (kata ya Nar) , Utwari na Umagi kata (Madunga),na Maabara za Shule za sekondari za Dabil na Dareda.
Pia Timu hiyo ilitembelea Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Msingi Wallahu kata ya Bashnet, na zahanati za Vijiji vya Mandi na Sabilo.
Madhumuni makuu ya ya ziara hiyo ni kuwaelekeza viongozi wa kata na Vijiji umuhimu wa kufuata taratibu za manunuzi katika kutekeleza miradi hiyo na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza miradi hiyo.
Kiongozi wa Timu hiyo Ndg Benitho Kavenuke ambaye ni Afisa Mipango Halmashauri aliliwashukuru wananchi na uongozi mzimma wa Kata na Vijiji kwa kujitolea na kusimamia kikamilifu miradi hiyo.
Aidha wananchi wa Kata ya ya Secheda ,Madunga Kupitia kwa Diwani wao Michael Basso Ginyamati na Diwani wa Madunga Mhe.Noya,John Slvini wameishukuru serikali kwa kutoa fedha kuendeleza miradi ya Maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.