Friday 27th, December 2024
@KATA YA MAGUGU
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg Hamisi Iddi Malinga amewashukuru wafadhili wa shirika la Heart and Hands for Humanity Organisation kutoka Marekani wanaojenga visima vya maji katika Shule ya Msingi Mapea na Shule ya sekondari Magugu zilizoko Kata ya Magugu Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mkurugenzi Mtendaji ametoa shukurani hizo alipotembelea Shule ya Sekondari ya Magugu iliyoko Kata ya Magugu katika Halmshauri ya Wilaya ya Babati na kuwakuta wafadhili hao wanaendelea na utafiti ili waanze uchimbaji wa kisima kirefu cha maji katika shule hiyo.Naye Mkuu wa shule hiyo Ndg Hamis Maginga amemweleza Mkurugenzi Mtendaji kuwa kukamilika kwa kisima hicho kutasaidia kupunguza tatizo la maji
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.