Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka maofisa Habari kuandika kila mara habari zenye hamasa na kuibua ushuhuda kuhusu kazi na miradi inayotekelezwa na Serikali. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo kwenye kikao kazi na Maofisa Habari kilichofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma mjini Mtumba." Nendeni mkaisemee miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yenu" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amesema ipo miradi mingi ya sekta za Elimu, Afya,Utawala kilimo,Maji Barabara ambayo imetekelezwa nendeni mkaisemee kwa wananchi. Sambamba na hilo amewataka maofisa Habari hao kwenda kuandaa Vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii vitakavyoangazia kazi na miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.. Kikao kazi za Maofisa Habari kimeitishwa na Mhe Waziri Mchengerwa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu , kukuza taaluma ya habari na kuimarisha ushirikiano kati ya TAMISEMI na Taasisi zake
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.