Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda ameagiza Watendaji wa Kata na Vijiji kutoa Elimu na kuhamasisha Wananchi juu ya kujiunga na mpango wa Serikali wa Bima ya Afya kwa Wote. Mhe. Kaganda ameyasema hayo leo kwenye Kikao Maaluum cha kamati ya usimi klichofanyika katika Ukumbi wa H/ Wilaya ya Babati ili kuweka mpango kazi wa utoaji Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote ktk Halmashauri."Wataalamwa Afya Watendaji wa Kata na Vijiji suala la Bima ya Afya kwa Wote libebwa kwa nguvu zote liweze kufanikiwa" amesisitiza kiongozi huyo.Katika mpango huo kaya itachangia Tsh 150,000 na watu 6 kwenye familia watahudumiwa kwa mwaka. Wajumbe wa kikao hicho wameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha mpango huo kwani utasaidia kuongeza umri wa kuishi wa Mtanzania na kuwezesha kundi kubwa la Wananchi kupata huduma bila kikwazo cha fedha. Bima ya Afya kwa Wote ni Mpango unaowezesha Wananchi wengi kujumuishwa katika utaratibu wa kuchangia kabla ya kuugua na Serikali kuweka utaratibu kwa Wananchi wasio na uwezo kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.