Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewapongeza Wananchi wa kata ya Mamire kwa kuchangia kiasi cha Tsh 8 Million katika ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwikantsi. Mhe Kaganda ameyasema hayo leo kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa Madarasa 2 na Ofisi Moja katika shule hiyo. "Nawaopongeza kamati ya maendeleo ya kata na Wananchi wote wa kata ya Mamire kwa kuchangia katika ujenzi wa Shule hii" amesisitiza kiongozi huyo. Akiwa katika Shule hiyo ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya kutafuta fedha na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa Madarasa hayo ifikapo tarehe 30/01/2026. Wakati huo huo Mhe Kaganda amepiga marufuku Wananchi kukata miti ya asili kwa ajili ya ujenzi akiwaleza Wananchi kuwa malekezo ya Serikali kutunza mazingira. " Sisi sote tunahimizwa kutunza mazingira " amesisitiza kiongozi huyo. Katika ukaguzi huo Mhe Kaganda ameongozana na Viongozi wa kamati ya Ulinzi na usalama Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.