Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Angellah Kairuki amesema hatasita kuwachukulia hatua stahiki kwa wale wote watakaovuruga na kufuja fedha za Mradi wa uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi (Boost). Waziri ameyasema hayo leo kwenye hotuba yake uzinduzi wa Mradi huo kwa wajumbe wa timu ya utekelezaji wa Mradi huo kutoka Halmashauri za Mikoa ya Manyara ,Singida na Arusha yaliyofanyika leo Ktk Shule ya Sekondari ya llboru Mkoani Arusha " Nyinyi kama watekelezaji Wakuu hepukeni Rushwa" amesisitiza kiongozi huyo. Aidha amesema kuanzia Sasa kwenda kuhamasisha Jamii na wazazi kupeleka watoto kuandikishwa darasa la Awali na la kwanza Kwa mwaka 2023. Mradi wa Boost unatekelezwa Kwa Halmashauri 184 Kwa muda wa miaka 5 na utajenga Madarasa 12000 , Shule mpya kwa vijiji/ Mitaa ambayo haina Shule na utagharimu jumla ya trillion 1.15. fedha za kitanzania
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.