Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Selemani Jafo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Wananchi wa Kata ya Magugu kwa usimamizi mzuri wa ujenzi mpaka kukamilika kwa kituo cha Afya Magugu. Waziri Jafo ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kuweka jiwe la uzinduzi wa kituo cha Afya Magugu kilichopo kata ya Magugu katika H/W ya Babati, "Wananchi wa Magugu wameitendea haki fedha iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Pombe Magufuli kiasi cha Tsh Million 400 na leo tunaona majengo yote yamekamilika na yanatoa huduma."Binafsi nimefarijika sana hongera sana Wananchi wote wa Magugu" Amesisitiza kiongozi huyo.Aidha amewapongeza watumishi wa kituo cha Afya Magugu kwa utoaji huduma na akawaeleza kuwa anataka kituo cha Afya Magugu kiwe kituo Bora nchini. Katika hafla hiyo amekagua kituo na kuongea na Wananchi na kusisitiza kulinda amani na utulivu na kujiepusha na Rushwa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.