Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa Mhe. Dkt Harryson Mwakyembe amepongeza mazingira Mazuri ya Shule ya Sekondari Ayalagaya na Kusisitiza ujenzi wa viwanja vya Michezo ili Vijana waweze kucheza na kujipatia ajira. Hayo ameyasema leo tarehe 10/07/2018 akiwa kwenye Ziara ya kikazi katika shule ya Sekondari ya Ayalagaya kata ya Ayalagaya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara,"Jamii na taasisi ni lazima wajenge viwanja vya Michezo ili kuweza kuinua vipaji vya Vijana ni kupitia Michezo Vijana wanajipatia ajira na kuongeza kipato"Amesisitza Waziri huyo. Aidha amesisitiza Waajiri kugharamia Walimu wa Michezo kwenda kusoma na kuongeza ujuzi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.