Wazazi wa watoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wamesisitizwa kutimiza wajibu wao katika kusimamia malezi yaVijana ili kujenga jamii imara inayowajibika. Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg Halfan Mtapula kwenye Kongamano kuhusu mmomonyoko wa maadili na Malezi . Katika Hotuba yake iliyosomwa na Januari Bikuba Afisa Maendeleo ya Jamii H/ Wilaya ya Babati kwenye Maadhimisho ya siku ya familia Duniani iliyoadhimishwa Ki / halmashauri katika ukumbi wa chuo Cha Veta Dareda Katika hotuba hiyo, Ndg Bikuba aliomba, Viongozi wa Dini , Serikali na NGOs kuendelea kutoa Elimu juu ya mmomonyoko wa maadili na malezi. Aidha amesisitiza familia kudumisha upendo ili kuwa na familia imara zitakazowezesha watoto kupata malezi bora. Kongamano hilo limehudhuliwa na Viongozi mbalimbali na mada juu ya familia na malezi zimetolewa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.