Watumishi wa kada za afya , Fedha, Mipango na TEHAMA wametakiwa kutekeleza vizuri, Mipango, Direct health Financial Facility, ICHF iliyoboreshwa ili kutoa huduma nzuri na katika jamii. Akifungua mafunzo kwa Watumishi wa kada hizo Katika Ukumbi wa White Rose Mjini Babati, kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Ndg. A. Kaganda amesisitiza Watumishi hao kuwa makini kuhakikisha wanaelewa vizuri kwani ndiyo watakuwa Walimu katika Halmashauri zao.Mafunzo hayo pia yanalenga kuelimisha Jamii kupata dawa kupitia mfumo mpya wa jaJAZIA Prime Vendor Supplier (PVS) , mfumo huu utatumika kujazia dawa na vifaa tiba kwa haraka pale ambapo MSD itakwama kutekeleza jukumu hilo kwa haraka. Mafunzo Hayo yamehudhuriwa na Watumishi wa kada tajwa hapo juu kutoka Halmashauri sita za Mkoa wa Manyara.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.