Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Eng. Raymond Mushi amewataka Wafanyakazi kufanyakazi kwa bidii, kujituma na kuacha uvivu ili kuiletea nchi maendeleo. Mhe. Raymond ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi iliyofanyika mjini Babati katika viwanja vya Kwaraa ambapo amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Akijibu Risala ya Wafanyakazi iliyosomwa na Katibu wa Tucta Mkoa wa Manyara amesema ni kweli Tanzania ina ukosefu wa ajira hii ni kutokana na maendeleo ya Teknolojia na ukosefu wa viwanda na hii itapungua taratibu kutokana na ujenzi wa viwanda unaoendelea nchini. Aidha amewaomba Wafanyakazi kuhamasisha wananchi kulipa Kodi ili nchi ipate mapato na kuendeleza miradi yake. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mkoa na kupambwa na maonesho mbalimbali kutoka kwa Wafanyakazi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.