Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emanuela Kaganda amesisitiza Wananchi kufanya mazoezi ili kujikinga na Magonjwa. Mhe Kaganda ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa club ya Mazoezi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati uliofanyika leo katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Babati. " Serikali inasisitiza Watumishi kufanya mazoezi Ili kujikinga na Magonjwa kama kisukali, pressure na mengine mengi amesitiza kiongozi huyo. Aidha ameagiza Watumishi kwenye taasisi zao kuunda vikundi vyao na kufanya mazoezi kila mara . Kabla ya kuzindua club hiyo Mhe. Kaganda ameshiriki na Watumishi hao kufanya mazoezi.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.