Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu ameagiza Watendaji wa Vijiji na kata kusikiliza na Kutatua kero za wananchi katika maeneo yao. Hayo ameyasema leo kwa kwa nyakati tofauti wakati ametembelea na kujitambulisha katika Kamati za Maendeleo za kata za Kisangaji, Mwada, na Magugu "Sikilizeni kero na tatua kero mlizo na uwezo nazo zile ambazo hamna uwezo nazo zipeleke kunakohusika" amesisitiza Mkuu wa Wilaya. Aidha amesisitiza kuhakikisha wanazuia mimba za utotoni kwa wanafunzi katika maeneo yao.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.