Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Babati limeridhia rasmu ya Mpango na Bajeti wenye Tsh 71,343,150 ,000 kwa mwaka 2026/2027.Akiwasilisha Taarifa ya rasmu hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Kaimu Mkuu wa Division ya Mipango na Uratibu Emmanuel Lyimo amesema kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Halmashauri inatarajia kukusanya na kupokea Tsh 71,343,150,000 kutoka vyanzo vya Mapato ya ndani matumizi ya kawaida, mishahara , miradi ya maendeleo na wadau Maendeleo walioko katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Vilevile amesema Mpango na Bajeti huo umeandaliwa Kwa kuzingatia Sheria. Miongozo, ya uandaaji wa Mpango huo na kuzingatia maagizo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vipaumbele vya Halmashauri. Aidha Ndg Lyimo ameeleza kuwa Bajeti hiyo imejikita katika utekelezaji wa mkakati wa kuinua Wananchi kiuchumi, kuongeza ukusanyaji wa Mapato ya ndani na ujenzi wa miradi ya Maendeleo.Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. John Noya amesisitiza fedha iliyopangwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani inakusanywa na kupelekwa kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo kama iliyopangwa
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.