Washiriki wa Michezo ya UMISETA wametakiwa kujiamini kujituma na kushirikiana ili kufanya vizuri ktk Michezo ngazi zote. Hayo yamesemwa na Ndg Anna Mbogo Mwenyekiti wa UMISETA ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati leo katika ufunguzi wa Mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Ayalagaya " katika Mashindano haya wekeni nidhamu mbele ,jiamini na mjitume ili mfanye vizuri " amesisitiza kiongozi huyo. Mashindano hayo yanafanyika ktk ngazi ya H/Wilaya na yanashirikisha Michezo mbalimbali kv Riadha, mpira wa Miguu, netball, na Michezo mingine na fani za ndani, Timu zinazoshiriki ni Washindi kutoka kwenye kata ktk kanda tano za Mbugwe, Dareda, Bashnet, Gorowa na Babati . Washindi wa Michezo hiyo watashiriki Michezo ngazi ya Mkoa .
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.