Mkuu wa Wilaya Babati Mhe. Lazaro Twange ameipongeza H/Wilaya ya Babati kwa utekelezaji wa Sheria ya Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi ya Mfuko wa Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu. Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo makao Makuu ya H/ Wilaya Babati-Dareda wakati akikabidhi pikipiki 25 kwa vikundi vinne zilizonunuliwa na H/ Wilaya ya Babati kupitia mfuko huo ili kuwakopesha vijana."Pikipiki hizi tunawakopesha mnatakiwa kuzitunza vizuri ili ziweze kuwaondoa kwenye wimbi la umasikini na kuwaongezea kipato" amesisitiza kiongozi huyo. Mkurugenzi Mtendaji wa H/ Wilaya ya Babati Anna Mbogo amesisitiza vijana hao kufuata maelezo ya mkopo huo na kufanya marejesho kwa wakati ili vijana wengine waweze kukopeshwa.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.