Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wametakiwa kuuenzi, kuuthamini na kuendeleza Mila na tamaduni nzuri za Mtanzania kwa maendeleo yao, Jamii na nchi kwa ujumla. Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Ndg .Hamisi Malinga kwenye kilele cha Tamasha la Utamaduni Shule za Sekondari Tarafa ya Babati katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kufanyika Shule ya Sekondari ya Gallapo Kata ya Gallapo "ninyi Wanafunzi ni lazima muthamini Mila na tamaduni zetu nzuri za mtanzania ili muwafundishe wengine waupende Utamaduni wetu wa Mtanzania na kuuendeleza" amesisitiza Mkurugenzi huyo.
Tamasha hilo lenye malengo ya kuhamasisha taaluma shule za Sekondari, kuhamasisha Sana'a za maonesho na Mapambano dhidi mimba za utotoni na lenye kauli mbiu "Michezo na Sana'a kwa maendeleo ya Elimu limeshirikisha shule za Sekondari tano ambapo kila shule imeonesha Michezo ya Riadha na Sana'a za maonesho mbalimbali na kuhudhuriwa na Viongozi, Walimu, na wananchi kutoka kata nne .Akitoa neno la shukurani kwa niaba Wakuu wa Shule, Mkuu wa shule ya Sekondari Gallapo Ndg Ramadhan Angonvi amesema Tamasha hilo limekuwa chachu ya wanafunzi kuhudhuria Shuleni kwa wingi na wanafunzi wameweza kuelewa mada mbalimbali zilizotolewa. Kabla ya kilele hicho Maofisa Elimu , Utamaduni, Michezo na Vijana wametembelea kila shule na kukutana na Walimu wa Wanafunzi na kuhimiza wanafunzi kusoma kwa bidii .Katika Tamasha hilo Mshindi wa Kwanza Ni Shule ya Sekondari Endakiso,kata ya( Endakiso) Mshindi wa Pili Gallapo Sekondari, na wa Tatu ni Shule ya Sekondari Ayatsea (kata Gallapo) ambao wamepata fedha taslimu, ngao na vyeti
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.