Viongozi ngazi mbalimbali wametakiwa kutoa elimu kwa wazazi kwenda vituo vya kutoa huduma kwa ajili ya kujifungua. Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mkuu Ndg Elizabeth Changendo leo kwenye washa ya utoaji Elimu juu ya Mila Desturi na tabia zinazoathiri utoaji wa huduma za afya ya uzazi iliyofanyika ktk ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Arri na kudhaminiwa na Shirika la USAID Afya yangu."Msisitizo wangu kila ninapokutana na wanawake na viongozi ngazi ya jamii ni wanawake wajifungulie hospitaliniamesisitiza kiongozi huyo . Naye mshauri wa maswala ya Jinsia na Huduma zenye Heshima na Staha wa Mradi wa USAID Afya yangu Bi Mary Rwegasira amesisitiza jamii inatakiwa kuhamasishwa na kuelimishwa kutumia vituo vya kutolea huduma wakati wote vilivyojengwa na serikali na taasisi mbalimbali.Washa hiyo umehudhuriwa na baadhi wataalamu , viongozi wa dini ,viongozi wa serikali kutoka tarafa nne za H/W ya Babati na kwa umoja huo wametengeneza mpango kazi wa uraghabishi wa jamii juu ya juu ya maswala ya afya
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.