Mkurugenzi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Babati Ndg. Anna Philipo Mbogo amewaomba wazazi kutumia Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali hasa za kujifungua. Mbogo ameyasema hayo leo Hospitalini hapo akiwa ameshikilia Mtoto Philipo George Zakalia akiwa mtoto wa kwanza wa kiume kuzaliwa katika wodi ya Wazazi ktk hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mwada. "Serikali ya inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imesogeza huduma karibu na wananchi tuzitumie kikamilifu hasa hospitali yetu ya H/Wilaya ya Babati amesisitiza kiongozi huyo. Wakati huo huo familia ya mtoto Philipo wamemshukuru Mkurugenzi Mtendaji na Uongozi wa hospitali kwa huduma nzuri na wakasema wameamua kumuita mtoto wao jina la "Philipo" ambalo ni jina la Baba yake Mkurugenzi ili kuenzi juhudi zake za ujenzi hospitali hiyo. Wodi ya Wazazi katika hospitali ya H/Wilaya imeanza kutoa huduma tangu tarehe 29/5 na huduma zingine zinaendelea wananchi wanakaribishwa kupata huduma bora katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.